Wednesday, November 2, 2011

Mwanza hali si shwar!

Kanisa la Tanzania Assemblies of God 

2 comments:

  1. Mwanzo wa tatizo:
    Mama mmoja aliombewa na vijana wa kanisa la TAG huko eneo la Iloganzala Mwanza .Alikuwa anasumbuliwa na mapepo na kufanyiwa shughuli za uganga bila mafanikio lakini baada ya kuombewa yale mapepo yalimtoka yule mama.
    Ndipo alipoamua kubadili dini na kuanza harakati za kusali ktk kanisa hilo lakini wale vijana wakamuambia kuwa iwapo ataendelea kubaki na zile hirizi alizopewa na waganga itakuwa ni kivutio kizuri kwa mapepo yale kumrudia tena na kufanya makazi kwake. Ndipo walipomuomba kwa hiari yake wazichome hirizi zote na madawa mengine aliyopewa kama kinga dhidi ya yale mapepo. Kabla hawajachoma yule mama aliwaambia kuwa kuna makaratasi yamebandikwa ukutani na huwa akiyaona hayo makaratasi moyo humruka na kuenda mbio na ndipo alipowaambia kuwa wayatoe yale makaratasi yote yaliyokuwa ukutani ambayo yalikuwa yameandikwa lugha ya kiarabu na alipewa na wale waganga ili ayabandike kama kinga.
    Baada ya tukio hilo la kuchoma hivyo vitu vyote ndipo alipofika kijana wake na kumuuliza Mama yake kwanini wamechoma makaratasi yaliyoandikwa kwa lugha ya ''kiislamu'' (kama alivyodai kijana mwenyewe), na ndipo yule kijana kwa hofu ya imani yake akakimbilia msikitini na kutoa taarifa na baada ya muda kidogo sauti toka kipaza sauti cha msikiti kikawaita waislamu wote na wakakusanyika na baadhi ya viongozi wao wakaenda hadi kwa mkuu wa wilaya na mkoa kutoa malalamiko yao bila hata kufuatilia na kujiridhisha kwa taarifa iliyoletwa na muumini wao kama ni kweli ama la!

    Usiku huo waumini hao wa kiislamu walichoma makanisa manne (4) na ndipo mgogoro ulipozidi. Mnamo siku ya jumanne trh 11/10/2011 kundi la waislamu walijipanga na petrol na vitu ambavyo vilihisiwa kuwa ni mabomu wakiongozwa na sheikh wa mkoa kulipua ama kuyachoma makanisa na ndipo taarifa zilipomfikia IGP Said Mwema na kutumia msaidizi wake alimpigia simu mufti na kumuambia amuonye sheikh wa mkoa wa mwanza juu ya kile walichopanga kufanya usiku ule wa 11/10/2011 na baadaye msaidizi huyo wa mwema alimpigia simu sheikh wa mkoa wa mza na kumuambia afanye jitihada zote kuwafikishia ujumbe aliowapanga kutekeleza tukio hilo waache mara moja na kumwambia iwapo kanisa hata moja litachomwa moto..........(hakumalizia kauli)....na kweli uhalifu huo haukutekelezwa

    Vurugu za leo:

    Baada ya makanisa yale manne kuchomwa sheria ilichukua mkondo wake na watuhumiwa walitiwa nguvuni ikiwa ni pamoja na waliochoma vile vitu na baadhi ya nyaraka zilizodaiwa kuwa ni Quran na baada ya utulivu kurejea walipewa dhamana lkn waislamu waliapa kuwaua kwani walidai hao watu wana malengo ya kuumaliza uislam.

    Leo ilikuwa ni siku ya kesi na ilitarajiwa hukumu lakini tarehe imesogezwa mbele ambavyo nami bado sijapata sababu hadi sasa,hali hiyo iliamsha hisia za watu wengi ambao wengi wao walikuwa ni waumini wa dini ya kiislamu na jazba kupanda na kuanza kwa fujo na mapambano na askari.
    Hii fujo ya leo ilikuwa imeratibiwa kwa muda sasa kwani nami nilipata taarifa ya kufanyika kwa fujo hii hiyo jana na ndicho kilichofanyika

    ReplyDelete
  2. 5.3 Wajibu kwa Jamii

    Tutatoa taswira kwa taifa na ulimwengu tukidhihirisha upendo na haki ya Mungu katika maneno na matendo yetu.

    5.4 Kufanya kwa Pamoja (Kwa timu)

    Mahusiano ya upendo yatatawala kila eneo la maisha ya kanisa hii ikijumlisha dhana ya huduma itokanayo na msukumo wa upendo. Huduma zinazotimizwa kwa pamoja (kitimu) na kujenga ushirikiano.

    ReplyDelete