Monday, April 21, 2014

Kuitambulisha Bajaj RE 4S Mpya

Jukwaa linalotembea la Experiential Marketing, likitoa elimu na burudani maeneo ya Mbagala jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya sifa muhimu za Bajaj RE 4 S ni hizi zifuatazo:
1. Mfumo wa injini wenye plagi mbili pacha.
2. Injini ina pistoni moja na valvu mbili.
3. Mfumo wa injini wenye mapigo manne kwenye chemba ya aluminiamu.
4. Ina kipoza injini chenye mfumo wa hewa na oili.
5. Chasisi imara zaidi.
6. Kebini imeongezewa nafasi zaidi.
7. Ina sehemu ya kuchaji simu.
8. Ina kihifadhi cha chupa ya maji.
9. Kizuia matope kimetengenezwa kwa chuma.
10. Nafasi katika uvungu ni sentimeta ishirini.
Sifa hizi na nyinginezo nyingi zinakupa ubora na thamani ya pesa yako.