Friday, August 26, 2011

East African News Agency-Disemba 2010

        
Katibu Mtendaji wa Bonde la Ziwa Victoria( LVBC), Dk. Tom Okurut aliwaambia 
washiriki wa kongamano la uwekezaji katika bonde la ziwa Victoria, mjini Mwanza:
Uwekezaji katika uendeshaji wa rasilimali ya maji utazuia uharibifu na kuimarisha 
matumizi sawa ya rasilimali hiyo, Shirika la Habari la Afrika Mashariki (EANA) 
lilimnukuu Dk. Okurut akiwaeleza washiriki wa kongamano hilo.
Wajumbe wa kongamano hilo lililojumuisha wawekezaji wa sasa
na wawekezaji watarajiwa walielezwa vivutio mbalimbali vya uwekezaji 
vilivyopo katika bonde la ziwa Victoria na jinsi gani vinaweza kuvunwa
na kubadili maisha ya watu wanaoishi kuzunguka ziwa hilo.
 Wajumbe walisema uimarishwaji wa teknolojia ya mawasiliano na habari 
utawezesha kukuza uwekezaji katika kanda hiyo.
Wakizungumzia juu ya utafiti, wajumbe hao waliitaka sekta binafsi 
na taasisi za fedha kuanzisha sera ya utafiti na maendeleo ya kanda.
Ili kukuza utalii, wajumbe walisema, kuwepo na juhudi za pamoja za kutafuta soko 
na kukuza utalii wa ndani ya Bonde la Ziwa Victoria.
Ziwa Victoria ni kubwa kuliko maziwa yote barani Afrika, 
kubwa kuliko yote katika ukanda wa tropiki duniani 
na ni ziwa la pili ulimwenguni lenye maji baridi 
likitanguliwa na ziwa Superior lilipo Amerika ya Kaskazini.
Baadhi ya vivutio vilivyomo ndani ya ziwa Victoria ni pamoja na:
kuwepo kwa visiwa 88 kati ya hivyo 48 ni visiwa vikubwa 
ambavyo vinaweza vikawa ni miongoni mwa maeneo ya utalli, 
yapo maeneo ya mapumziko na fukwe zinazoweza kuendelezwa kwa utalii 
na ipo nafasi kubwa ya kuanzishwa kwa viwanda vingi vya minofu ya samaki.















Wednesday, August 17, 2011

Nyumbani

Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki.
Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati na misemo, mithali na mashairi , mafumbo , vitendawili na nyimbo.
Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika nchi zifuatazo:
  • Tanzania: Lugha ya taifa; ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani; inatumika kote nchini, kanisani, kwenye misikiti, kwa redio, runinga na idadi kubwa ya magazeti.
  • Kenya: ni lugha ya taifa lakini Kiingereza ni lugha rasmi ya Kiutawala; Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo penye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani zinatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu la Kiswahili; sehemu za programu redioni na kwenye runinga ni kwa Kiswahili. Lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au kikabila. Hata hivyo baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa mnamo tarehe 4, Agosti 2010, Kiswahili sasa kitakuwa lugha rasmi, sawa na Kingereza.
  • Uganda: imetangazwa kuwa lugha ya kitaifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya kitaifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo. Ni lugha ya polisi na jeshi hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wananchi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakisema Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumika na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani.
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa, pia lugha ya jeshi katika mashariki ya nchi. Kiswahili kimefika na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani la Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Shaba

Tuesday, August 9, 2011

Welcome!


Welcome to Nyanza Information Centre website.

Nyanza Information Centre
NICE" is a new venture in the provision of information and communication technology. Translated in sukuma,"nyanza" means the lake.
The way lake Victoria links the East Africa nations, Nyanza Information Centre is a platform which aims at uniting people using innovative communication technologies. The Internet is becoming the most reliable and fast network, through which people of the lake region can interact with others in Africa; and the rest of the World.
The Vision Statement for the business is to become an ICT service provider with a skilled and equiped technical team.
The services will address the current market needs and wants. These include, internet services at a better download speed and reliability, training on business application, web advertising, and the print media.
The centre aims at making the exchange of ideas and current news in the form of text, voice and visual data a reality and affordable to cross cutting network groups.


Main Business Activities
Services - Internet Services

Karibu!

Mpendwa Msomaji,

Ninayo furaha kukukaribisha katika web log hii.
Lengo letu ni kukutanisha watu mbalimbali ndani na nje ya ukanda wa ziwa Victoria.
Tukitambua ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano na biashara, upo umuhimu wa kubadilika kulingana na tabia nchi, mazingira na makuzi.
Katika hatua hii ya mwanzo, tunathamini ushirikiano wako ili kukamilisha azma yetu, na kutimiza ndoto yako.
Matarajio yangu ni kwamba, wigo huu utaziba pengo la upashanaji habari kwa wajasiriamali na soko la ndani na nje kwa bidhaa zizalishwazo au huduma wanazotoa.
Pia, watumia huduma na wanunuzi wa bidhaa watafaidika kwa kuhabarishwa upatikanaji kulingana na mahitaji yao.
Kwa utangulizi huu mfupi, tena nasema karibu ujisikie huru kikamil!