Thursday, July 26, 2012

Maonyesho ya Wajasiriamali Mwanza.

Juma lilopita kuanzia Jumanne tarehe 17 Julai 2012, kulikuwa na maonyesho ya wajasiriamali wa kati na wadogo (SME's) katika ukumbi wa Jiji (Gandhi Hall).
Yaliandaliwa na Klabu ya BDG ( Business Development Gateway) Mkoa wa Mwanza.
Bidhaa na Huduma mbalimbali zilikuwepo, kama: Vyakula asilia vya lishe vilivyosindikwa, soya, matunda, Mvinyo wa mlonge na lozera, dawa na sabuni za usafi, nguo za kike na kiume, bidhaa za ngozi kama mikanda, viatu na mabegi, pia huduma za teknolojia ya habari na mawasiliano, dagaa waliokaushwa, mashine za kusaga na kukoboa nafaka, misumeno na landa za mbao, majiko bora na sadifu, pia mitambo ya kubadili mfumo wa umeme ( DC/AC Inverter).
Siku ya Ijumaa tarehe 20 Julai 2012, niliweza kupata picha kama unavyoweza kuona hapa: