Friday, December 6, 2013

Jinsi ya kununua gari kutoka Japan

Broshua hii itakupatia maelezo ya namna unavyoweza kununua gari moja kwa moja kutoka Japani, Marekani au Korea ya Kusini. 
Orodha ya ofisi za wawakilishi waliopo karibu nawe pia imewekwa kwa ajili yako mteja.
Kwa maoni yoyote ili kuboresha, tafadhali tuandikie.


Thursday, December 5, 2013

Mradi wa kujengea uwezo wajasiriamali wadogo na wa kati (SME)

Kila mwaka, benki ya KCB Tanzania imekuwa ikiendesha semina kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.
Mradi ambao hujulikana kama SME Capacity Building Project. Jijini Mwanza, semina hii ilifanyika pale JB Belmont Hotel siku ya tarehe 21 Novemba, 2013.
Washiriki mbalimbali, wengi wao wakiwa ni wateja wa KCB Bank Tanzania Limited walihudhuria.
Ilikuwa ni yenye manufaa kwa kila mpenda maendeleo.
Pichani: Mkurugenzi wa Nyanza Information Centre, Musa George akipokea cheti cha ushiriki.