Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati na misemo, mithali na mashairi , mafumbo , vitendawili na nyimbo.
Kiswahili kimekuwa lugha rasmi katika nchi zifuatazo:
- Tanzania: Lugha ya taifa; ni lugha ya shule za msingi, lugha ya utawala serikalini na mahakamani; inatumika kote nchini, kanisani, kwenye misikiti, kwa redio, runinga na idadi kubwa ya magazeti.
- Kenya: ni lugha ya taifa lakini Kiingereza ni lugha rasmi ya Kiutawala; Kiswahili ni lugha ya kwanza ya mawasiliano kati ya wananchi wakikutana nje ya eneo penye kabila moja tu; ni lugha inayofundishwa lakini si lugha ya kufundisha mashuleni; ni lugha inayotumika na polisi na jeshi, ni lugha ya kuhutubia wananchi mjini na kitaifa; sehemu za ibada makanisani zinatumia Kiswahili; kuna gazeti moja tu la Kiswahili; sehemu za programu redioni na kwenye runinga ni kwa Kiswahili. Lugha inachanganywa mara nyingi na Kiingereza na lugha za maeneo au kikabila. Hata hivyo baada ya rasimu ya katiba mpya kupitishwa mnamo tarehe 4, Agosti 2010, Kiswahili sasa kitakuwa lugha rasmi, sawa na Kingereza.
- Uganda: imetangazwa kuwa lugha ya kitaifa tangu 2005; iliwahi kuwa lugha ya kitaifa wakati wa utawala wa Idi Amin; wakati wa ukoloni ilifundishwa mashuleni ikaelekea kuwa lugha rasmi pamoja na Kiingereza lakini matumizi haya yalipingwa hasa na Waganda hivyo Waingereza waliacha mipango hiyo. Ni lugha ya polisi na jeshi hali ambayo imeleta ugumu kwa lugha kukubalika na wananchi wengi kutokana na historia ya utawala wa kijeshi Uganda; watu wengi bado hukumbuka hasa matusi ya wanajeshi waliowatesa wakisema Kiswahili. Lakini kuna maeneo ya Uganda ambako Kiswahili kinatumika na watu wengi kama lugha ya sokoni na barabarani.
- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: Kiswahili ni kati ya lugha nne za kitaifa, pia lugha ya jeshi katika mashariki ya nchi. Kiswahili kimefika na misafara ya biashara ya watumwa na pembe za ndovu kutoka Zanzibar na pwani la Tanganyika. Imeenea zaidi kati ya mchanganyiko wa wafanyakazi kwenye migodi ya Shaba
No comments:
Post a Comment