Katibu Mtendaji wa Bonde la Ziwa Victoria( LVBC), Dk. Tom Okurut aliwaambia washiriki wa kongamano la uwekezaji katika bonde la ziwa Victoria, mjini Mwanza: Uwekezaji katika uendeshaji wa rasilimali ya maji utazuia uharibifu na kuimarisha matumizi sawa ya rasilimali hiyo, Shirika la Habari la Afrika Mashariki (EANA) lilimnukuu Dk. Okurut akiwaeleza washiriki wa kongamano hilo. Wajumbe wa kongamano hilo lililojumuisha wawekezaji wa sasa na wawekezaji watarajiwa walielezwa vivutio mbalimbali vya uwekezaji vilivyopo katika bonde la ziwa Victoria na jinsi gani vinaweza kuvunwa na kubadili maisha ya watu wanaoishi kuzunguka ziwa hilo. Wajumbe walisema uimarishwaji wa teknolojia ya mawasiliano na habari utawezesha kukuza uwekezaji katika kanda hiyo. Wakizungumzia juu ya utafiti, wajumbe hao waliitaka sekta binafsi na taasisi za fedha kuanzisha sera ya utafiti na maendeleo ya kanda. Ili kukuza utalii, wajumbe walisema, kuwepo na juhudi za pamoja za kutafuta soko na kukuza utalii wa ndani ya Bonde la Ziwa Victoria. Ziwa Victoria ni kubwa kuliko maziwa yote barani Afrika, kubwa kuliko yote katika ukanda wa tropiki duniani na ni ziwa la pili ulimwenguni lenye maji baridi likitanguliwa na ziwa Superior lilipo Amerika ya Kaskazini. Baadhi ya vivutio vilivyomo ndani ya ziwa Victoria ni pamoja na: kuwepo kwa visiwa 88 kati ya hivyo 48 ni visiwa vikubwa ambavyo vinaweza vikawa ni miongoni mwa maeneo ya utalli, yapo maeneo ya mapumziko na fukwe zinazoweza kuendelezwa kwa utalii na ipo nafasi kubwa ya kuanzishwa kwa viwanda vingi vya minofu ya samaki. | ||
Friday, August 26, 2011
East African News Agency-Disemba 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment