Tuesday, December 31, 2013

Tunapoaga mwaka 2013

Hii ilikuwa ya aina yake >


Tarehe 29 Julai 2013 ilikuwa siku ya mwisho wa mkutano wa injili katika Kanisa la Nazarene lililoko Kiseke, jijini Mwanza. Pichani ni sehemu ya igizo lililohusu mfano wa Yesu wa kusamehe, kati ya watumwa wawili.

1 comment:

  1. Mathayo 18: 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

    21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?

    22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

    23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.

    24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta

    25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.

    26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

    27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.

    28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari

    29 Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

    30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.

    31 Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.

    32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;

    33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?

    34 Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.

    35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

    ReplyDelete